July 9, 2018


Kocha Mkuu wa Yanga, raia wa DR Congo, Mwinyi Zahera, ametamka kuwa beki wa pembeni wa Singida United, Michel Rusheshangoga, ndiye mchezaji wa kwanza aliyependekeza kwenye orodha ya majina aliowapendekeza katika usajili wake kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Kauli hiyo aliitoa hivi karibuni wakati kocha huyo akijiandaa kutangaza orodha ya wachezaji waliosajiliwa na kuachwa kwenye usajili wa msimu huu wiki hii.

Timu hiyo hivi sasa ipo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa straika Mkongo, Haeritier Makambo, Deus Kaeseke na Mrisho Ngassa.

Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Zahera alisema alikuwa anamfuatilia beki huyo kwa karibu tangu muda mrefu na kuvutiwa na kiwango chake kikubwa lakini amefuta mipango ya kumsajili beki huyo baada ya kupata taarifa ya kusajiliwa na APR ya Rwanda.

“Katika msimu uliopi­ta wa ligi, nilivutiwa na wachezaji watatu pe­kee kutoka nje ya timu ya Yanga na kati ya hao yupo beki wa pembeni wa kulia wa Singida, raia wa Rwanda.

“Kiukweli ni mchezaji mzuri mwenye uwezo mkubwa wa kukaba na kupeleka mashambulizi kutokea pembeni ambaye yeye jina lake nililipeleka kwa uongozi na kuniambia kuwa ameondoka Singida na kwenda kusaini APR.

“Pia, wapo wachezaji wen­gine wawili ambao majina yao siyafahamu vizuri kama unavyofahamu mimi ni mgeni, hivyo sifahamu wachezaji wengi majina yao,” alisema Zahera.

1 COMMENTS:

  1. Saleh unajitekenya na kuruka mwenyewe sio!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic