SAMATTA SASA KUMFUATA LIONEL MESSI
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania na KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta yupo kwenye mazungumzo na Klabu ya Levante inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania ‘Laliga’ kukamilisha mpango wa kuhamia klabuni hapo.
Levante imetenga kitita cha Euro milioni 4 ili kumnasa Samatta, japo klabu yake anayoitumikia KRC Genk, imekataa ofa hiyo na kuhitaji Euro milioni 8. Iwapo atafanikiwa kutimkia huko, basi atacheza Ligi moja na mwamba wa soka wa Dunia, Lionel Messi wa Barcelona.
Wakala wa Samatta amethibitisha kuwepo kwa mazungumzo baina ya klabu hizo mbili huku miamba ya Urusi klabu ya CSKA Moscow imekuwa ikihitaji huduma ya kijana huyo Mtanzania.
Samatta lipojiunga na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea katika miamba ya soka ya Afrika, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
0 COMMENTS:
Post a Comment