BASATA WAMZUIA DIAMOND KWENDA KUFANYA SHOO NJE
BARAZA la Sanaa Tanzania (BASATA) leo limemzuia mwanamuziki, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwenda kufanya shoo nje ya nchi akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa sababu msanii huyo hakuwa na kibali.
Kaimu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Onesmo Mabuye alipokuwa akizungumza na TBC, kuhusiana na sintofahamu hiyo kuwa ni kutokana na msanii huyo kukosakibali cha Basata.
BASATA wamesema kwa sasa hivi kuna utaratibu mpya ni kuwa msanii akitaka kwenda kufanya shoo nje ya nchi ni lazima apitie kwa BASATA wampe kibali na kisha akirudi pia anatakiwa kuripoti kwao
BASATA wamesema kumzuia Diamond wanataka iwe fundisho kwa wasanii wengine ili wanapoenda nje ya nchi wafuate taratibu zilizowekwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment