July 6, 2018


Unaikumbuka ile staili ya mpapaso waliyokuja nayo Ruvu Shooting FC katika Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18? Basi msimu ujao wanakuja na nyingine ambayo ni mara mbili yake.

Sasa mambo yako hivi. Kwa mujibu wa Msemaji anayetamba kwa kuwa na maneno mengi zaidi kuliko wasemaji wote Tanzania, Masau Bwire, amefunguka na kueleza kuwa katika msimu ujao watakuja kivingine zaidi.

Bwire amesema ili kuwapa shida wapinzani katika ligi itakayokuwa na timu 20 zitakazokuwa zinashiriki, wamepanga kuja na staili inayokwenda kwa jina la Mpapaso Square (Mpapaso Sikwea) ikiwa na maana ya kuwa watakuwa wanapapasa zaidi ya mara moja ndani ya mechi moja.

Bwire ameeleza wameamua kuandaa mfumo huo ili kuleta changamoto kubwa kwa ajili ya kupigania kikombe cha Ligi Kuu Bara na kujionesha kuwa wapo tofauti na timu zingine hapa Tanzania.

Mbali na aina hiyo ya uchezaji, Bwire ameziponda pia timu ambazo zimekuwa zikisajili kwa mbwembwe akisema huo ni usajili wa sifa wala hauna maana yoyote ile.

Mbali na kuponda, Bwire amesema klabu yao ya Ruvu Shooting imekuwa ikifanya usajili wa kipekee kwa kuzingatia matakwa ya timu, na akieleza lazima waje na moto katika msimu wa 2018/19.

Msemaji amefunguka na kueleza hayo bila kuzitaja klabu husika ambazo zimekuwa zikiendelea na usajili kwa ajili ya kuboresha vikosi vyao, akisema hakuna la maana ambalo wanafanya na badala yake wategemee ushindani wa hali ya juu kutoka kwa Ruvu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic