July 27, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa Yanga umetangaza rasmi kuachana na wachezaji kadhaa waliokuwa wakiichezea timu hiyo msimu wa 2017/18 ambapo kuelekea msimu ujao hawatakuwa na kikosi cha klabu hiyo.

Wachezaji hao ni Donald Ngoma ambaye amejiunga na Azam FC, Godfrey Mwashiuya aliyetimkia Singida United, Hassan Kessy na Obrey Chirwa.

Yanga imeweka wazi juu ya wachezaji hao baada ya kushindwa kufikia nao makubaliano hapo awali ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo ambayo ndiyo bingwa wa kihistoria katika Ligi Kuu Bara.

Wakati wakitangaza kuachana na wachezaji hao, Yanga imewaomba mashabiki na wanachama wake wajitokeze kwa wingi Jumapili hii katika Uwanja wa Taifa kuipa hamasa timu.

yanga itakuwa inacheza kibarua cha mashindano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Gor Mahia FC kutoka Kenya ukiwa ni mchezo wa mkondo wa pili.

Katika mechi ya awali iliyochezwa jijini Nairobi, Kenya, Yanga ilikubali kichapo cha mabao 4-0 kwa bila na kuzidi kujipa matumaini hafifu ya kuendelea kusalia kunako mashindano hayo ya CAF.

4 COMMENTS:

  1. Yanga twende kwa wingi sana kwasababu lakwanza kuliko yote ni kuvuna pesa nyingi kutokana na madeni tuliyonayo kwani imefika hadi hata kambi ya Morogoro ikatushinda na pili angalau bughudha tunazofanyiwa mitaani zipunguke na timu ipate morali na kupata ushindi tuliokuwa kila mechi. Pia tunataka voongozi wapya wawe wabunifu dio kumtegemea myu mmoja ambae alitumia mabiloni na mwisho wake yalipomzonga akaitua yanga na akatia pamba mashikioni. Tuishi kama walivoishi watani wetu tulipokuwa tunawanynganya nyota kutokana na umasikini wao nao hawakutetereka na walivmilia na hatukuyaona yale yanayotusibu sasa

    ReplyDelete
  2. duh Kessy kapigwa chini.Ama kweli msaliti husalitiwa.Aliondoka Simba kwa mbwembwe.Sasa hana hata benchi la kukaa!

    ReplyDelete
  3. KLABU YA YANGA INAHUJUMIWA YAANI KUNA "KIRUSI" PALE YANGA SIJUI NI NANI INAWEZEKANA MTANDAO HUU UMESUKWA KWA MUDA MREFU...UNAMUHUSISHA KOCHA MWINYI ZAHERA, HIVI HUYU KOCHA ATAWEZAJE KUKATAA BEKI AMBAYE ANAKUJA KUZIBA MAPENGO YA NAMBA 2 NA TANO? UNAACHA WACHEZAJI, HALAFU UNAPEWA BEKI MZIMBABWE BURE HALAFU UNAMKATAA...KWELI? HAYA UNAWAACHA WACHEZAJI AMBAO WAMEKUHUDUMIA MSIMU MZIMA KWA KUTOLIPWA MSHAHARA.....BADO HAUJAFANYA USAJILI WA KUZIBA MAPENGO YA WACHEZAJI WALIONDOKA...BEKI NAMBA 2 NA 5, WASHAMBULIAJI NAMBA 9, 10, 11, KIUNGO NAMBA 6....HALAFU UNATAKA WATANZANIA ASILIMIA 55% AMBAO NI WAPENZI WA KLABU WAJE UWANJANI, KUANGALIA TIMU IPI? NATABIRI MAPATO YA UWANJANI KUPOROMOKA, HAMASA YA KWENDA KWENYE MECHI KUPUNGUA....HATIMA YA SOKA LA TANZANIA KUPOROMOKA..

    ReplyDelete
  4. Kessy aliihujumu Simba kwenye mechi na Yanga wakati anaichezea Simba. Laana ile imeendelea. Ameshindwa kuvumilia kuitumikia Yanga kipindi ambacho Yanga ina matatizo ya fedha. Mbona wenzie Tambwe wamevumilia?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic