July 3, 2018


Wakati ikielezwa kuwa Deus Kaseke amesaini mkataba wa miaka miwili Yanga, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, ameibuka kivingine.

Nyika amefunguka na kueleza kuwa bado hajaingia mkataba na Kaseke ambaye siku chache zilizopita ilielezwa tayari ameshamalizana na mabosi wa klabu hiyo tayari kuitumikia Yanga msimu ujao.

Mwenyekiti huyo ambaye amezungumza akionekana kama kulificha suala hilo, amesema hakuna suala kama hilo japo akieleza kama watafanikiwa kumalizana na Kaseke basi watalitangaza hapo baadaye.

Ikumbukwe awali Kaseke aliripotiwa kuwa anaelekea Afrika Kusini kujiunga na klabu mojawapo nchini humo lakini mambo yakaenda tofauti na sasa ameanza kuhusishwa kwa kasi kumalizana na Yanga.

Kaseke aliondoka Yanga kuelekea Singida United pamoja sambamba na aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mholanzi, Hans van der Plujim mwishoni mwa msimu wa 2016/17 .                                                                                                                                                                                                                                                                          

4 COMMENTS:

  1. Nyie mzubae na kukanusha tu ati siri na Manara mwenye busara nyingi na kipaje cha ajabu atapotmtupia mshipi na chambo kitamu na kumnasa mseme mnaonewa

    ReplyDelete
  2. MJINGA UMEDHIBITIWA SAFARI HII, UTABAKI NA TAARIFA ZAKO ZA KUUNGAUNGA TU

    ReplyDelete
  3. Haya yetu masikio na ukimya wa Yanga.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  4. Yanga wanafanya usajili wa kimyakimya sasa hiyo ya Kaseke vipi tena

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic