Ofisa Habari wa klabu ya APR ya Rwanda, Clever Kazungu, amefunguka na kumuelezea Haji Manara kama mtu mwenye kipaji cha aina yake katika uzungumzaji anapokuwa anawasilisha jambo.
Kazungu amemtaja Manara ambaye ni Ofisa Habari wa Simba akisema ana kipaji cha aina yake katika uzungumzaji huku akisema anamkubali kutokana na kazi anayoifanya kwenye klabu ya Simba.
Kiongozi huyo kutoka APR amemueleza Manara kuwa utofauti wake na yeye kuwa ana uwezo wa kuzungumza maneno mengi huku akisema wanaendana katika kuwasilisha ujumbe kwa umma.
Kazungu amesema Manara anastahili kuwa hivyo kutokana ukubwa wa klabu yake akiamini kuwa pale mtu anapokuwa msemaji wa timu kama Simba ni lazima uwe vile.
Ofisa huyo ambaye pia ni Mwanahabari mkongwe yupo hapa nchini kwa ajili ya michuano ya KAGAME ambapo jana timu yake iliweza kufungwa mabao 2-1 na Simba katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Manara yupo sawa hasa katika kurejesha hamasa katika mchezo wa soka ila nabii siku zote huwa taabu sana kukubalika kwenye jamii inayomzunguka.
ReplyDeleteManara is a man of social nature, wise, abliest team's statesman, lovely, popular and with very convincing flow of ideas, who no one can corner him.
ReplyDeleteMANARA ALISOMA KWA PESA ZA YANGA NA HATA UMAARUFU WAKE UNATOKANA NA JINA LA BABAAKE AMBAE ALIKUA MCHEZAJI WA YANGA ILIBIDI ALIPE FADHILA ZA YANGA BADALA YA KUIPONDA !!
ReplyDeleteManara alisoma kwa pesa za baba yake siyo za Yanga kwa sababu mzee Manara alikiwa mfanyakazi qa Yanga(mchezaji)na alishawahi kucheza Simba pia,usilazimishe aisemee vizuti Yanga wakati moyo wake hautaki
DeletePumba
DeleteManara kazaliwa anaishabikia Simba hata pale baba yake mchezaji wa yanga. Wakati yeye mdogo kwa jinsi alivokuwa haipendi yanga alichukua buti za baba yake na kuzitia ndani ta ndoo iliyojaa maji ili baba yake ashindwe kuichezea yanga. Lini Manara alifadhiliwa na yanga?
ReplyDelete