July 5, 2018



Uongozi wa aklabu ya Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, umefunguka na kueleza juu ya suala la aliyekuwa Mwenyekiti wake, Yusuf Manji, kuchelewa kujibu barua ya kuombwa atengue maamuzi ya kujiuzulu wadhifa wake.

Nyika ameeleza kuwa bado Manji kweli hajajibu barua yao na ikumbukwe katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa klabu hiyo waliazimia kupinga kujiuzulu kwake na kupendekeza aendelee kuwa Mwenyekiti wao.

Mwenyekiti huyo amefafanua kwa kusema yawezekana labda akawa ametingwa na majukumu yake binafsi kikazi hivyo mpaka sasa hawajaweza kujua ni lini ataweza kuijibu.

Aidha, Nyika ameeleza itawibi wazidi kumpa muda mpaka pale atakapopata nafasi ya kuwajibu kwa maana hivi sasa bado hakuna chochote ambacho imewafikia kutoka kwake tangu wamtumie barua hiyo.

Kupitia Kamati ya kuipigania Yanga wakati wa Mpito, Nyika amesema inaendelea kufanya kazi ya kusaka fedha kwa ajili ya kuisaidia Yanga ili iweze kufanya usajili na kuiwezesha klabu kuhusiana na ulipaji wa mishahara ya wachezaji.

Nyika ameielezea kamati hiyo kuwa si kwamba inatoa fedha bali inafanya mipango ya kutafuta watu watakaotoa fedha ili klabu ili iweze kutekeleza majukumu yake ikiwemo usajili na mengine.


7 COMMENTS:

  1. Hebu jiongezeni, Manji angekuwa na nia ya kuendelea kuwa mwenyekiti isingechukua muda wote huo kutoa tamko. Kimyakimya Fc mmeachwa mbali sana ki fikra na Mzee Akilimali, japo siungi mkono kwa huyu mzee kuwa kiongozi wa Yanga lakini ana vision kuliko hao wenye mamlaka. Msitegemee mtu, tengezeni mfumo ambao utavuta watu sahihi bila kiwalamba miguu. Mnajidhalilisha sana pamoja na nembo ya club yenu. Povu mkafulie soksi na jezi za wachezaji wenu.

    ReplyDelete
  2. Vuteni subira, atawajibu kimya kimya

    ReplyDelete
    Replies
    1. Atawajibu Kimya Kimya ???????? Hii mpya !!!!!

      Delete
  3. Yaani ni majanga tu, where is the solution?

    ReplyDelete
  4. HIVI AKILIMALI HUWA MNAMTUMIA MUDA GANI VILE! WAJINGA MNASHIDA NYIE.

    ReplyDelete
  5. Nimekywa daima nikijiuliza kwanini yanga imefika hadi ya kujidhalilisha bila ya kuona aibu ambayo haijatokea tokea kuanza tarehe ya mpira hapa Tanzania. Inaonesha wazi kuwa katika yanga wapo ambao wakiitegemea yanga kuendesha maisha yso na kwa sasa kutoweka hela ya Manji kwao ni msiba na ndio hso walookodi daladala kwa maelekezo ya wajanja hadi kwa Manji kumramba miguu, lakini manji hakutoka kuonana nao na bado hawajakata tamaa, aibu gani hii. Glorious death is better than a shameful life. Mara mamolooni ya Manji yameingia, mara tunsfanya usajili wa siri na mwisho kumbe hamna chochote

    ReplyDelete
  6. Lol makubwaa. ..Badala ya kutafuta mfumo mbadala bado kuna ndoto za Alinacha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic