YANGA YAWATUMIA SALAAM HIZI SIMBA KUELEKEA MSIMU WA 2018/19 LIGI KUU BARA
Wakati Simba wakitamba kuwa watautetea ubingwa walioutwaa katika Ligi Ku bara msimu ujao, Yanga wameibuka na kueleza kuwa wanajiandaa kurejesha kikombe chao.
Ofisa Habari wa klabu hiyo, Dismas Ten, amefunguka na kusema kuwa kwa sasa wanakiandaa kikosi chao katika hali ambayo itawapa presha watani zao wa jadi Simba baada ya kufanikiwa kuneka kombe msimu wa 2017/18.
Ten ameeleza kuwa kwa sasa wameshaweka mikakati maalum ya kuhakikisha Yanga inarudi kwa kasi ili kuweza kuonesha utawala wake ndani ya soka la hapa nyumbani ili kuhakikisha ubingwa unarejea kwao msimu ujao.
Yanga ndiyo mabingwa wa kihistoria mpaka sasa kwa kulibeba taji hilo mara 27 huku Simba wakiwa wamechukua mara 19 tangu kuanzishwa kwakwe.
Katika msimu uliopita, Yanga ilimaliza msimu ikiwa imejikusanyia jumla ya alama 52 pekee nyuma ya Azam iliyokuwa na 58 wakati huo mabingwa Simba wakiwa na 69.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteWATU WAMECHOKA NA AHADI....HIZI LUGHA TUNAPANGA, TUKO KWENYE MCHAKATO, TUNAJIANDAA, WATU WAMECHOKA, WATANZANIA SIO WAPUMBAVU KUWADANGANYA KWA KIASI HICHO. KAMA HAMNA HABARI YA KUTOA KWA WANAWAHOJI SIO LAZIMA KUJIBU.....WAAMBIENI BADO MPAKA TUTAKAPOKUWA TAYARI TUTAWAAMBIA
ReplyDeleteWacheni porojo lisilokuwa na uhai. Wachwzaji wanatimkia kwenye maisha na wengi wao wanakataa mkataba mipya. Kwa jinsi mulivo jitayarisgeni luporomoka bila ya breki. Manji kakimbia anaona mtamfilisi. Alipokutakeni mlimkataa na sasa mnamtaka yeye hakutakeni tena. Mmemshika tu bila hata kiona aibu
ReplyDeleteYANGA WASIPOANGALIA WANAWEZA WAKAFANYA VIBAYA KWENYE MCHEZO WAO NA GOR MAHIA ZIMEBAKI WIKI MOJA NA NUSU LAKINI BADO ASILIMIA KAMA 70% YA WACHEZAJI WA KIKOSI CHA KWANZA HAWAJAANZA MAZOEZI, WENGI WAO WAKIWA WANADAI MISHAHARA NA MIKATABA MIPYA AMBAYO BADO HAWAJAPEWA HII NI HATARI SANA, MWALIMU AMEANZA MAZOEZI NA KUNDI KUBWA LA WACHEZAJI WAPYA WANAOJARIBIWA, HII NI HATARI SANA, HATA HUYO MANJI KAMA ANA NIA NZURI YA KUISAIDIA YANGA KWANINI ASIRUDI TU KWENYE KAZI NA KUWALIPA MADAI YA WACHEZAJI? HIVI YEYE ATAFURAHI IKIWA TIMU HAITASAFIRI KWENDA KENYA KWAKUWA WACHEZAJI WAMEGOMA?? KWELI KAMA NIA YAKE NI NZURI KWANINI AISIINGILIE KATIKA WAKATI HUU AMBAPO MUDA UNAZIDI KWISHA, NA HAO WACHEZAJI HATA MAZOEZINI HAWAENDI??? HIVI HIYO KAMATI KWANINI HAIFANYI YALE WALIYOAMBIWA WAYAFANYE KATIKA MKUTANO MKUU? MUDA UNAISHA NA HAKUNA LINALOENDELEA NI VURUGU TUPU? HIVI KOCHA KWANINI ANAWAKATAA WACHEZAJI WANAOJARIBIWA? NA KWANINI HATA WANACHAMA HAWAUSHINIKIZI UONGOZI WAFANYE JUU CHINI WACHEZAJI WAANZE MAZOEZI HARAKA KWANI MUDA UNAISHA????
ReplyDelete