August 4, 2018


Mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele, 21, amekuwa akijivinjari na wachezaji wa Arsenal wakati wa likizo , na kuongeza uvumi kwamba huenda akajiunga na the Gunners. (Goal.com)

Ajenti wa kipa wa Chelsea Thibaut Courtois ameitaka Chelsea kumwachilia mchezaji huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 26, kuhamia katika klabu ya Real Madrid. (Sun)

Liverpool ina hamu ya kumsaini kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey, 27, kutoka Arsenal. (Express)

Mshambuliaji wa Ufaransa na Manchester United Anthony Martial, 22,huenda akasalia katika klabu hiyo ya Old Trafford kwa kuwa mkufunzi Jose Mourinho hataki kumuuza hadi atakapopata mchezaji mbadala kuchukua mahala pake. . (Mirror)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Michy Batshuayi, 24, ananyatiwa na miamba ya Uhispania Atletico Madrid. (L'Equipe - in French)

Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery ana mpango wa kumnunua beki wa Croatia na Besikitas Domagoj ,29,Vida kwa dau la £25m. (Sun)


Winga wa Monaco na Algeria Rachid Ghezzal, 26, anatarajiwa kujiunga na Leicester kwa dau la £12.5m. (L'Equipe - in French)

Mkufunzi wa Crystal Palace Roy Hodgson anasema kuwa atabisha mlango wa Chelsea ili kumsaini kiungo wa kati wa Uingereza Ruben Loftus-Cheek, 22. (talkSPORT)

West Ham wameimarisha hamu yao ya kutaka kumnunua winga wa Brazil Bernard, 25, ambaye bado hajapata klabu baada ya kutoka Shakhtar Donetsk mwisho wa msimu uliopita (Guardian)

Kutoka BBC


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic