August 4, 2018


Kiungo wa zamani wa Yanga, Abdi Kassim ‘Babi’ amefunguka kuwa amefurahia kitendo cha timu yake ya zamani cha kuandaa mchezo wa kumuaga aliyekuwa nahodha wake, Nadir Haroub ‘Cannavaro.’

Cannavaro amestaafu kuichezea timu hiyo na sasa amepewa kazi ya umeneja kwenye kikosi hicho.

Babi ameyasema hayo kufuatia Yanga kuandaa mchezo wa kirafiki dhidi ya Mawenzi Market ya Morogoro ambayo anaichezea kiungo huyo utakaopigwa Agosti 12, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

“Kwanza nawaambia mashabiki huu ni mchezo maalumu umewekwa kwa ajili ya Cannavaro kutoka uchezaji kwenda hatua ya umeneja wa timu na mambo ya uongozi kiujumla, kwa hiyo kwangu binafsi ninafurahi sana kukutana na Yanga maana mimi nitakuwa kwa upande wa Mawenzi Market na mechi itakuwa nzuri.” alisema.

Katika hatua nyingine, Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten alisema kuwa, kabla ya mchezo huo kutakuwa na burudani ya muziki kutoka kwa Mr Blue, Afande Sele, Lulu Diva, Juma Nature na Billnas huku Yanga Queens ambayo itaongozwa na Wema Sepetu itacheza na Morogoro Kombaini.

5 COMMENTS:

  1. Bora mngelichaguwa timu yenye kiwango na vilevile ya kujipima tayari kwa mechi zijazo za ubingwa kuliko kutafuta kitimu kihafifu almuradi mshinde tu.

    ReplyDelete
  2. Ni jambo zuri ILA nitamani viongozi vitafute mechi nyingine kwa Zanzibar ilitumuage vizuri shajaa wetu sliteitumiakia timu yetu kwa uadilifu mkubwa

    ReplyDelete
  3. Wabongo nyi kazi yenu si kupinga kila kitu kupinga tu watafutie basi timu wacheze nayo

    ReplyDelete
  4. HAKUNA TIMU INAYOITWA YANGA QUEENS ILA KUNA YANGA PRINCESS....BOYA WEWE

    ReplyDelete
  5. Yanga SC ni kama hawana viongozi wenye kufikiria kwa kutumia akili. Andaeni mechi na timu ya level zenu then sehemu ya mapato ya viingilio mumkabidhi Cannavaro.

    Fanyeni promo ya kutosha na sisi mashabiki & wapenzi tutakuja uwanjani kwa ajili ya shujaa wetu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic