BAADA YA KUKOSA MDHAMINI MANARA ASEMA LIGI ITAKUWA YA TIMU MBILI, AWATAKA TFF WAMTAFUTE AWAPE UJANJA WA KUMPATA
Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, amesema kuna dalili kubwa ya msimu ujao ligi kwa na washindani wakubwa wawili ambao ni Simba na Azam FC.
Hatua hiyo imekuja kufuatia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kukosa wadhamini wakuu wa ligi mpaka sasa baada ya Kampuni ya Mawasiliano Vodacom kumaliza mkataba wake.
Kwa mujibu wa Radio EFM kupitia Sports HQ, Manara ameeleza Azam na Simba wanaweza kuleta ushindani pekee kutokana na kuwa vizuri kiuchumu tofauti na klabu zingine ambazo zinapitia changamoto kifedha.
"Kwa namna hali ilivyo kwa timu nyingi kuna uwezekano mkubwa ligi inaweza ikawa na ushindani wa klabu mbili pekee ambazo ni Simba na Azam, hivi vingine vina hali ngumu itakuwa changamoto kwao".
Aidha, Ofisa huyo amewashauri TFF waendelee kupambana kumsaka mdhamini ili aweze kuja kuwa suluhisho la matatizo kwa timu zingine huku akisema kama inawezekana wamtafute ili awasaidie kumtafuta.








Tatizo katika usimamizi wa wa michezo Tanzania ni kubwa mno na la kusikitisha. Karia alikuwa chini ya utawala uliofeli wa Malinzi. Waliomueka madarakani Karia ni wale wale watu waliomueka madarakani Malinzi. Kwa hiyo utawala wa Karia ni muendelezo wa utawala wa Malinzi na ndio maana utaona Tanzania imeshindwa kupiga hatua yeyote ile ya viwango vya soka Duniani tangu karia waingie madarakani. Ni vigumu kuwashawishi wadhamini makini chini ya uongozi wa staili ya Karia. Moja ya kitu ambacho TTF imefeli na itaendelea kutufelisha ni suala la usimamizi wa timu ya Taifa Stars. Namuheshimu sana Amunike lakini sikubaliani hata kidogo na uteuzi wake wakuwa kocha mkuu wa taifa stars yaani kama masihara vile wakati suala la kocha wa timu ya taifa ni suala nyeti na sio la kukurupuka. Amunike ni kocha mwanafunzi yaani yupo katika hatua za kujiendeleza kitaaluma na sio kocha Nguli na kuna uwezekano mkubwa wa Amunike kuchukua muda kabala ya kujua nini cha kufanya wakati timu tayari inakabiliwa na mashindano tofauti na kocha mzoefu. Mtu au mtanzania unaweza ukajiuliza masuali mengi sana juu ya TFF na hasa katika uteuzi wa makocha na usipate majawabu. Mfano kocha aliekuwa wa Yanga Mzambia Lwandamila kati yake na Amunike nani mwenye uzoefu wa ukocha zaidi wakuweza kututoa hapa tulipo? Nadhani kila mtanzania atanielewa nini nazungumza. Kiushabiki mimi ni mnyama wa kupoteza fahamu ninapoguswa na machungu lakini lakini kama kuna kocha Mtani alipatia basi Lwandamila. Yule jamaa ni bonge la kocha asikwambie mtu na hapana shaka angetufaa sana hata kwa Taifa Stars. Chini ya Lwandamila nnaimani Taifa Stars isingekuwa kichwa cha majaribio ya wanaotaka kujifundishia kunyoa. Ndio pale tunapouliza kwanini mchakato wa kocha wa Taifa Stars unakuwa wa siri na si wazi watu wakatoa maoni yao? Waache wadhamini wakimbie kudhamini ligi yetu kwani mdhamini yeyote hawezi kuacha kudhamini ligi ambayo timu yake ya Taifa wachezaji wake anaowadhamini kwenye ligi watamngaza zaidi kimataifa. Ligi gani iliokuwa haina timu ya taifa?
ReplyDeleteTiefu efu ni sawa na kichefu chefu..!!
ReplyDelete