August 17, 2018


Zikiwa zimesalia siku chache kuelekea kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu Bara nchini, Katibu Mkuu wa zamani wa Yanga, afunguka juu ya kukosekana kwa mdhami mkuu.

Siku mbili zilizopita Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, lilisema ligi ya msimu ujao itaanza bila mdhamini mkuu ambaye wanaendelea kuzungumza naye.

Kitendo hicho kimefanya Tiboroha kuibuka na kusema kuwa si jambo jema kwa mpira wa Tanzania kutokana na kuwa na chombo ambacho kinasimamia mpira wa soka la nchi.

Kwa mujibu wa Radio One, Tiboroha ameeleza kuwa klabu nyingi zitakuwa zimeathirika na kukosekana kwa mdhamini huyo ambaye amekuwa akivisaidia ili kuweza kujikimu kwa masuala mbalimbali ikwemo gharama za kusafiri.

Tiboroha ambaye ni Mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), anaamini itakuwa changamoto kubwa kwa timu hizo ambazo zimekuwa zikipigana kutokana na hali ngumu kiuchumi kuzikumba.

Aidha, Tboroha ametoa ushauri akivitaka kufikia hatua ya kutafuta wadhamini wake badala ya kutegemea wadhamini wakuu wa ligi ikiwemo kubadili mifumo ya uendeshwa kutoka wa kizamani kwenda wa kisasa.

Hatua hiyo imekuja baada ya klabu nyingi kujikita na utegemezi wa wadhamini wakuu wa ligi ambao mpaka sasa hawajapatikana jambo ambalo lisineleta matatizo endapo timu zenyewe zingekuwa katika mfumo wa kisasa au kuwa na wadhamini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic