BAADA YA KUKOSA NAMBA MANCHESTER, JOE HART ATIMKIA ZAKE BURNLEY
Aliyekuwa golikipa wa Manchester City, Joe Hart, amejiunga na Burnley kwa kusaini mkataba wa miaka miwili.
Hart amekamilisha uhamisho huo wenye thamani ya pauni £3.5m ikiwa na baada ya kukosa namba ndani ya mabingwa hao wa Ligi Kuu England.
Kwa muda mrefu Hart amekuwa akihaha kupata timu ambayo itamuwezesha kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza baada ya Man City kushindwa kumtumia.
Kipa huyo alikosa namba Man City baada ya kocha Pep Guardiola kusema hana mipango naye ya kumtumia katika kikosi cha kwanza cha timu yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment