Habari njema kwa wateja wa DStv, kuwa Kampuni ya Multichoice kwa mara ya kwanza wataanza kushuhudia Ligi ya Italia ‘Serie A’ ambayo itaonyeshwa mubashara kupitia DStv.
Hiyo, ikiwa ni siku chache tangu kumalizika kwa Kombe la Dunia 2018 baada ya wateja wake kupata burudani ya soka kupitia DStv na hivi sasa wateja wataweza kuangalia mechi zaidi 1200 katika msimu huu mpya wa soka.
Hamasa imeongezeka katika msimu huu mpya wa soka ni kuonyesha Serie A ni baada ya mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo kusaini Juventus ya Italia wakiamini macho ya mashabiki wa soka yataelekeza huko.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika uzinduzi huo wa msimu mpya wa soka, Meneja Uendeleshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo alisema, wateja wapya sasa wataweza kujiunga na DStv kwa shilingi 79, 000 ili kupata seti nzima ya king’amuzi cha DStv na kufurahia msimu wa soka.
“Mbali ya kufurahia matangazo kwa lugha adhimu ya Kiswahili katika Ligi Kuu ya Uingereza, wateja wa DStv wataweza pia kuangalia DStv popote wakati wowote kwa kutumia vifaa kama simu na kompyuta.
“Wateja wataangalia soka kwa kupitia simu zao za mkononi au compyuta kwa kupakua program yetu ya DStv Sasa, unaweza kutumia hadi vifaa vitano tofauti ambavyo vinaunganishwa na ‘decoder’ yako ambayo huwawezesha wanachama wa familia kuangalia program tofauti kwa wakati mmoja.
“SuperSport ni nyumba ya soka na tunafurahia kuwa katika msimu mpya wa soka ndani ya DStv pekee ambapo Watanzania wataweza kushuhudia ‘live’ Ligi ya Uingereza, Serie A bila kusahau Ligi ya Hispania maarufu kama La Liga,” alisema Shelukindo.
Uzinduzi huo wa msimu mpya wa soka ulihudhuliwa na baadhi ya wachezaji wakongwe wa Simba na Yanga akiwemo Edibily Lunyamila, Mohamed Hussein ‘Chinga’, Sekilojo Chambua, Boniface Pawasa, Akida Makunda, Adolph Rishard na wasanii wa kundi la Weusi wakiongozwa Joh Makini na G Nako.
NITAFURAHIA ZAIDI WAKIONYESHA LIGI YA NYUMBANI VPL
ReplyDelete