August 31, 2018


Uongozi wa klabu ya Coastal Union ya Tanga, umesema umechelewa kutambulisha jezi zake mpya kutokana na kukumbwa na changamoto kadhaa.

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Coastal, Steven Mguto, amesema kwa sasa bado jezi zake hazina mdhamini baada ya watu waliokuwa wamekubaliana nao kuwa na majukumu mengine nje ya nchi.

Mguto amechukulia suala hilo kama jambo ambalo linaiumiza klabu na changamoto kubwa kwao, kwani walipaswa kuwa wameshakamilisha jambo hilo mapema kabla ya ligi kuanza.

Licha ya kushindwa kuwa na nembo na mdhamini wao, Mguto ameeleza kufikia Septemba 3 2018 tayari watakuwa na uzi wenye nembo za wadhamini wao.

Wakati Mguto akifunguka hayo, kikosi cha Coastal kipo kambini hivi sasa kikijiandaa na mechi zijazo za Ligi Kuu Bara ambapo mchezo ujao watacheza na KMC ya Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic