August 4, 2018


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amelazwa katika kituo cha afya Magugu akipatiwa matibabu zaidi kutokana na majeraha aliyoyapata katika ajali asubuhi leo akitokea mkoani Arusha kuelekea Manyara karibu na eneo la Magugu ambapo Ofisa wa habari, Hamza Temba amefariki dunia.


Katika ajali hiyo ya gari kulikuwa na watu sita akiwamo Waziri Kigwangalla ambaye ameumia katika mbavu, mkono na shingo. Kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu wilayani Manyara ambapo  pia wakiandaa utaratibu wa kumhamishia yeye pamoja na majeruhi wengine katika hospitali kubwa kwa matibabu zaidi.


3 COMMENTS:

  1. ALLAH awape shifaa ya haraka wore waliopat majeraha na amueke pema peponi marehemu

    ReplyDelete
  2. Sina uhakika na mazingira ya ajali hiyo ilivyotokea lakini watanzania wengi tulisisitiza sana kuwe na ulinzi wa hali ya juu kwa huyu muheshimiwa kutokana na jinsi anavyojitoa katika kuhifadhi rasilimali za taifa. Hivi karibuni alishawekewa mawe njiani katika moja ya misafara yake ya kazi wakasema ni vitu vya kawaida? Kigwangala mwenyewe ni moja ya rasimali muhimu kwa taifa anapaswa kulindwa kwa nguvu zote. Kigwangala ndio sababu leo tunaona muheshimiwa raisi anazidi kuwa na imani katika teuzi za vijana katika nafasi mbali mbali za kazi. Kingwangala ni mwanajeshi hasa aliejitolea muhanga kulipigania Taifa. Wizara yake ina maadui wengi wa nje na wa ndani nchi ni lazima apewe ulinzi wa kutosha. Moja katika vitu vya kushangaza kwa miaka mingi wanyama wamekuwa wakikrosi boda karibu kila mwaka kutoka Tanzania kwenda kenya na baadae kurudi Tanzania,lakini mara hii wanyama wamegoma kuondoka Tanzania kwenda kenya. Sababu zipo nyingi zinazotolewa kuhusiana na kisa hicho hadi kuipelekea kenya kuishutumu Tanzania kuwazuia wanyama hao kwenda kenya kwa madai ya kuchomwa moto kwenye njia ya wanyama hao ya kuelekea kenya. Lakini don't mistake kuwachukulia wanyama kuwa hamnazo yaani hawana akili hawajui nini kinachoendelea? Wanyama wanaakili ya asili pengine kushinda hata mwanaadamu na kuona vitu ambavyo mwanaadamu havioni na moja ya sababu ya kutokwenda wanyama kenya na kuamua kubaki Tanzania ni kutokana na amani inayorejea kwa nguvu katika mbuga zetu. Iwe ya kiusalama au ya wananchi kusita kuvamia mbuga za Taifa kulisha mifugo yao na kuongeza ziada ya malisho kwa wanyama pori, hiyo ni kutokana na kazi tukuka ya muheshimiwa Kigangwala tangu kushika waizara ile kwa muda mfupi. Watanzania hatuna kawaida ya kujivunia vizuri vya kwetu lakini huyu kigwangala ni wa kujivunia sana bila ya aibu ili kuwa na Tanzania yenye heshima.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hongera sana kwa nyama na madini uliyomwaga ndugu yangu

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic