JERRY AWAOMBEA YANGA MILIONI 100 KWA MO
Kuelekea tamasha la Simba Day tunapaswa kujifunza mengi kutokana na tamasha hilo la watani wetu wa jadi, kwanza kabisa tunapaswa kujifunza uzalendo wa kupenda vyetu na kusaidia wenzetu pindi msaada unapohitajika.
Watani zetu Simba nawapongeza kwa kuanzisha tamasha hilo 'Simba Day' kwani mmeonesha uzalendo mkubwa sana kwa timu yanu kwa kupitia tuzo mbalimbali mnazotoa kwa waliowahi kuitumikia klabu yenu"waasisi" hii inatia moyo kwa wachezaji na viongozi wenu kuweza kujituma ili kuipa simba mafanikio makubwa.
Pia kwa misaada mbalimbali mnayotoa kwa wahitaji kama vile yatima na wasiojiweza ni kitu muhimu sana kwa maisha ya kawaida ya kibinadamu na hili ndilo hasa lililonifanya niandike makala hii.
Napenda kuwashauri viongozi wa simba pamoja na mwekezaji wao bwana Mo Dewji kwamba msaada huo huelekezwe kweli kwa wahitaji na si kutoa kwa wasiokuwa na uhitaji wa msaada huo.
Kipaumbele changu katika msaada huo ni yatima na wasiojiweza na kama Bwana Mo akiwa vizuri zaidi ni vyema pia akawapatia msaada wa kipesa watani wake Yanga japo milion 100 kwani hiyo ni pesa ndogo sana kwa tajiri huyo kijana kwa Afrika ila kwetu sisi Young Africans ni kiasi kikubwa sana kutokana changamoto ya ukata wa pesa tunayopitia na akifanya hivyo hatomsahau maishani japo utani wa simba na yanga utaendelea milele lakini mungu atambariki kwa kuwa na moyo wa kusaidia wahanga mbalimbali.
Niwatakie maandalizi mema ya tamasha lenu
Jerry Murro A.k.A Mr Dc
Yanga Daima Mbele, Nyuma Mwiko
Imefika hadi yanga kuombewa msaada kutoka kwa mahasimu. Huenda Mo akatoa kwa ukarimu wake lakini jinsi ninavoijuwa yanga, pesa watapokea na siku ya mechi baina ya Simba na Kotoko mashabiki wa yanga wataizomea Simba pamoja na mechi zitazofata
ReplyDelete