August 4, 2018


Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Omary Kaaya amefunguka na kuwapa majibu wale ambao wamekuwa wakisema kuwa klabu hiyo imeanzishwa bakuli maalum kwa ajili ya kupokea michango.

Kaaya ameeleza kuwa utaratibu huo umekuwa wa kawaida kwa Yanga akisema hata Ulaya ni jambo la kawaida kwa timu zilizo chini ya wanachama kuzichangia timu zao.

Kaimu huyo amesema baada ya kuanzisha utaratibu huo wa kuichangia Yanga, ameeleza utakuwa ni mwendelezo utakaoenda kwa muda mrefu ambapo kila kitu kitakuwa na uwazi.

Uongozi wa Yanga uliitisha kikao jana na waandishi wa habari kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo la kuichangia klabu huku ukitoa maelekezo namna ambavyo wanachama na mashabiki wanaweza kutuma fedha kupitia namba maalum walizotoa.

Yanga imeamua kuanzisha mpango huo wa kukusanya michango kutokana na kipindi huki cha mpito inachopitia ili klabu iweze kujiimarisha kwa ajili ya kuhakikisha mambo mbalimbali yanakwenda sawia.

2 COMMENTS:

  1. Achana na wajinga weka number za simu. Tuanze kumwagia Timu yetu mapesa. Nashangaa ni kwanini tunapoteza muda wakati vijana wetu wanahitaji maisha mazuri.

    ReplyDelete
  2. Wengi tupo tayari kuisaidia timu yetu, lakini suala la mchango wa pesa za Sportpesa zikowapi na nyenginezo halijibiwi na imekuwa wengi tunaogopa pesa za bakuli nazo ikawa mambo ni hayo. Kwanini hawaweki wazi hata tukawa na imani?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic