KESSY AGEUKA MWEKUNDU BAADA YA KUTAMBULISHWA NKANA ZAMBIA
Aliyekuwa beki wa kulia wa klabu ya Yanga, Hassan Kessy, ametambulishwa rasmi na timu ya Nkana Red Devils inayoshiriki Ligi Kuu Zambia.
Kessy ametambulishwa na timu hiyo ikiwa na baada ya siku kadhaa zilizopita kusaini mkataba wa miaka miwili huku akikabidhiwa jezi namba 22.
Kessy alifikia makubaliano na Nkana baada ya mabosi wake wa zamani Yanga kushindwa kuelewana naye juu ya dau alilokuwa analitaka ili aweze kuongeza mkataba mpya.
Beki huyo aliwataka Yanga kumpatia kiasi cha milioni zaidi ya 70 pamoja na gari ili aendelee kuichezea klabu hiyo ambayo ni bingwa wa kihistoria ndani ya Ligi Kuu Bara.
Lakini Yanga walitia ngumu kwa kuendelea kumpa ahadi za polepole kuwa watakuja kumalizana naye lakini ilipofikia mwisho wa dirisha la usajili kufungwa wakampa taarifa kuwa hawawezi tena kumsajili.
Kesi kajikwamua peke yake bila ya kuwachukuwa kaka zake
ReplyDelete