Kocha mpya wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems, ameweka bayana dhumuni la kucheza na Asante Kotoko leo kwenye tamasha la Simba Day.
Aussems ambaye alikuwa na kikosi cha Simba nchini Uturuki kwa wiki mbili, anaamini mechi hiyo itampa mwangaza wa kuiandaa vizuri timu.
Kocha huyo aliamua kukifumua upya kikosi ambacho kilikuwa kipo chini ya Msaidizi, Masoud Djuma ambaye alichukua nafasi ya Mfaransa, Pierre Lechantre kwa muda, amesema mchezo huo utamsaidia kukiweka sawa kikosi chake kuelekea msimu ujao.
Aidha, Aussesm amesema Kotoko ni timu kubwa ambayo itakuwa ni kipimo kizuri kwa Simba kuelekea msimu ujao huku akieleza kuwa watajitahidi kupambana nayo ili tamasha hilo liweze kufana.
Simba inashuka dimbani majira ya saa 10 kukipiga na Kotoko ambao ni wakongwe wa Ligi Kuu Ghana ambapo hivi sasa wapo katika nafasi ya 4 katika msimamo wakiwa na utofauti wa alama 3 dhidi ya Ashanti Gold walio nafasi ya kwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment