August 16, 2018


Nyota wa Manchester City Kevin de Bruyne anachunguzwa zaidi kwenye goti lake la kulia baada ya kuumia akishiriki mazoezi Jumatano.

Ubaya wa jeraha hilo la kiungo huyo wa kati haujabainika kufikia sasa.

Mwaka 2016, alikosa mechi 12 baada ya kuumia goti lake la kulia wakati wa mechi ya nusufainali Kombe la EFL ambapo walipata ushindi dhidi ya Everton.

Kwa mujibu wa BBC, De Bruyne, 27, alitawazwa mchezaji bora wa msimu wa Manchester City msimu uliopita baada ya kuwafungia mabao 12 na kusaidia ufungaji wa mabao mengine 21.

Aliwasaidia City kushinda taji la Ligi ya Premia na Kombe la EFL.

City, walioanza kutetea taji lao kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Arsenal wamepangiwa kukutana na Huddersfield nyumbani kwao Jumapili.

Baadaye watacheza ugenini dhidi ya Wolves na kisha nyumbani dhidi ya Newcastle kabla ya mapumziko ya kimataifa.

Mechi yao ya tano ya msimu itakuwa nyumbani dhidi ya Fulham mnamo 15 Septemba kabla ya mechi yao ya kwanza hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 18 au 19 Septemba.

City walivunja rekodi kadha msimu wa 2017-18, ikiwa ni pamoja na kufikisha alama 100, na pia kushinda mechi 32 na kufunga magoli 106 msimu mmoja enzi ya Ligi ya England.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic