August 30, 2018


Kipa namba moja wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Aishi Manula, ameshindwa kujumuika na kikosi cha timu hiyo katika mazoezi yaliyoanza leo kwenye Uwanja wa Boko Veterani.

Manula ameshindwa kujumuika na wenzao kutokana na kusumbuliwa na majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City wakati akitumikia klabu yake ya Simba.

Kipa huyo amekuwa mchezaji pekee kati ya 7 kutoka Simba aliyewahi kuripoti kambini ili kuanza maandalizi ya kuelekea mchezo wa kufuzu fainali za AFCON dhidi ya Uganda, Septemba 8 2018.

Stars na Uganda zitakutana tarehe hiyo huko Kampala kupiga kipute hicho ambacho kinasubiriwa kwa hamu na wadau wengi wa soka la Tanzania na Uganda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic