Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amekuwa kivutio kikubwa cha wapenda soka mkoani Mtwara.
Ruvu Shooting iko hapa mkoani Mtwara tayari kwa ajili ya kuivaa Tandagimba City katika mechi ya kirafiki mjini hapa, kesho.
Masau ameongozana na kikosi hicho kwa ajili ya mechi ya kirafiki itakayochezwa kesho Jumatano kwenye Uwanja wa Makonga uliopo Newala mkoani Mtwara.
Mashabiki wengi walionekana kuwa na hamu kuu ya kumuona msemaji huyo matata.
Baada ya kuteremka kwenye basi la timu, walimfuata na kumsalimia huku wengine wakiomba kupiga naye picha.
Mechi hiyo itakuwa ni sehemu ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara msimu mpya wa 2018-19 lakini michuano mingine ndani ya msimu huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment