August 8, 2018


Wakati aliyekuwa beki wa klabu ya Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' kutangaza kustaafu soka, mchezaji aliyewahi kuichezea pia timu hiyo Athuman Idd Chuji ameshangazwa na maamuzi ya mkongwe huyo.

Chuji ambaye aliwahi kuitumikia Yanga kwa mafanikio na akifanikiwa kuchukua ubingwa miaka kadhaa nyuma na Yanga, amesema Cannavaro ameamua kupumzika mapema zaidi japo umri unamruhusu kucheza.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya mchezaji huyo kuteuliwa kuwa Meneja wa timu ya Yanga huku aliyekuwa akishikiria nafasi hiyo, Hafidh Saleh, akipandishwa cheo na kuwa Mratibu wa klabu.

Chuji ameeleza kuwa Cannavaro kwa umri ambao anao hivi sasa alipaswa kuendelea kusakata kambumbu lakini akisema hawezi kumsemea sana pengine maamuzi yake ni sahihi.

Mchezaji huyo ambaye sasa yupo Coastal Union ya Tanga anaamini Cannavaro ataindekea haki nafasi yake ya Umeneja ndani ya Yanga kutokana na uzalendo ambao anao katika klabu yake.

Beki huyo mstaafu ataagwa rasmi na Agosti 12 ambapo Yanga itacheza dhidi ya Mawenzi Market katika mchezo wa kirafiki huko Morogoro ambapo kikosi kimeweka kambi maalum kujiwinda na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger.


1 COMMENTS:

  1. Hii picha bora iondoshwe inatosha mpaka inatia karaha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic