MESSI, POGBA, GODIN, ROSE, HERRERA: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO JUMATANO
Mkurugenzi wa Barcelona Ariedo Braida anasema klabu yake haiwezi kutoa ofa kwa Paul Pogba wa Manchester United msimu huu, lakini amemtaja mchezaji huyo Mfaransa mwenye miaka 25 kama mchezaji mzuri na atakuwa anamfuatilia Mfaransa huyo. (Mirror)
Klabu ya Bundesliga ya Schalke wana mpango wa kutoa mikataba ya kudumu na hawana nia ya kuwasaini beki wa Tottenham raia wa England Danny Rose, 28, au kiungo wa kati wa England Ruben Loftus-Cheek, 22, kwa mkopo. (Sky Sports)
Meneja mpya wa Chelsea Maurizio Sarri amelegeza sheria kali kuhusu lishe na ratiba za mechi zilizowekwa na mtangulizi wake Antonio Conte. (Telegraph)
Sarri yuko radhi kiungo wa kati wa Chelsea mwenye miaka 28 Danny Drinkwater auzwe mwezi huu. (Star)
Lionel Messi hatacheza kwenye mechi yoyote ya Argentina na haijulikani iwapo mshambuliaji huyo wa Barcelona mwenye miaka 31 atacheza tena mechi za kimataifa. (Clarin - in Spanish)
Mlinzi wa Leicester mwenye miaka 25 Harry Maguire yuko karibu kukubaliana na mkataba wa pauni 75,000 kwa wiki kwenye klabu huyo. (Telegraph)
Wing'a wa Manchester City mwenye miaka 21 raia wa England Patrick Roberts anatarajiwa kujiunga na klabu ya Uhispania ya Girona kwa mkopo. (Sky Sports)
Meneja wa Arsenal Unai Emery atalazimika kufuata matumizi finyu ya fedha kwenye klabu msimu ujao kwa kununua wachezaji. (Telegraph)
Uwanja mpya wa Tottenham hatakuwa tayari ifikapo Novemba na klabu hiyo itakuwa ikichezea mechi zake zote za nyumbani huko Wembley. (Times - subscription required)
Kutoka BBC
0 COMMENTS:
Post a Comment