August 28, 2018


Wakati Yanga wakiwa wanasubiria kipute cha mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sports kesho, taarifa zinzasema Kocha wake Mkongomani, Mwinyi Zahera, ataelekea kwao Congo.

Licha ya kuwa na majukumu ya kuinoa Yanga, Zahera pia ni Kocha wa timu ya taifa ya Congo kama Msaidizi hivyo ataelekea huko kwa ajili ya kuwajibika kuiandaa timu kuelekea mchezo wa kufuzu AFCON.

Congo itashuka dimbani kucheza na Liberia Septemba 9 mwaka huu tayari kuanza kuchanga tiketi yake ya kupata nafasi ya kucheza AFCON ambapo pia Tanzania itakuwa inacheza dhidi ya Uganda Septemba 8 2018.

Baada ya Yanga kucheza na Rayon kesho, Zahera hataweza kurejea nchini na badala yake ataunga safari ya moja kwa moja kuelekea Congo ambapo timu ya taifa hilo Agosti 30 tayari kuanza maandalizi ya mechi hiyo.

1 COMMENTS:

  1. Au ndoo keshaingia mitini kachola kusubili hati yake ya kufundisha yanga?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic