August 28, 2018


Beki wa Uhispania na Barcelona Gerard Pique, 31, anasema itakuwa vyema sana iwapo kiungo wa kati wa Manchester United aliyeshinda Kombe la Dunia akiwa na Ufaransa Paul Pogba, 25, atahamia Nou Camp siku zijazo. (AS)

Beki wa England anayechezea Chelsea Gary Cahill, 32, yuko tayari kusalia na kupigania nafasi yake baada ya kuonekana kuwekwa pembeni katika kikosi cha Maurizio Sarri. (Telegraph)

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Ufaransa Thierry Henry, 41, anatarajiwa kuikataa nafasi ya kuwa meneja wa Bordeaux kwa sababu ya wasiwasi kuhusu ukosefu wa fedha katika klabu hiyo ya Ligue 1. (Sun)

Beki wa West Ham Reece Oxford, 19, anatafutwa kwa mkopo na klabu ya Eibar inayocheza ligi kuu Uhispania, klabu ambayo iko tayari kulipa ada ya £1.8m ya uhamisho wa mkopo. (Marca)

Kiungo wa kati wa Roma na Uholanzi Kevin Strootman, 28, anatarajiwa kufikisha kikomo kipindi cha miaka mitano ambayo amekuwa katika klabu hiyo ya Serie A na kuhamia Ufaransa kujiunga na Marseille kwa £22.6m. (Football Italia)

Kiungo wa kati wa zamani wa Chelsea na Brazil Ramires, 31, anakaribia kurejea klabu yake ya zamani ya Benfica kwa mkopo kutoka klabu ya China ya Jiangsu Suning. (O Jogo)

Los Angeles Galaxy wanamtaka beki wa zamani wa Arsenal na Ivory Coast Emmanuel Eboue, 35. (Sun)

Aston Villa wanajaribu kumshawishi mshambuliaji wa England Jack Grealish, 22, atie saini mkataba wa kudumu katika klabu hiyo inayocheza ligi ya Championship baada yao kukataa kumuuza Agosti. (Mirror)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic