August 17, 2018



Kwa kweli si vibaya kusema mkubwa! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ambaye alifanyiwa oparesheni kubwa ya moyo hali yake ya afya kuendelea vizuri na sasa ameshatoka hospitalini.


Mkwasa ambaye alijiuzulu nafasi yake hiyo hivi karibuni kisha majukumu yake yakakabidhiwa kwa Omary Kaaya, sababu ikiwa ni za kiafya, alienda nchini India Agosti Mosi na kufanikiwa kufanyia upas­uaji Agosti 4, mwaka huu.


Akizungumza kutoka India, mke wa Mkwasa, mama Betty Mkwasa alisema mumewe anaendelea vizuri kiafya na sasa wameshatoka hospitali na wapo kwenye hoteli lakini Mkwasa bado yupo chini ya uangalizi wa daktari ambaye anamhudumia.

“Anaendelea vizuri sana kiafya na sasa ame­shatoka hospitali, tupo hotelini licha ya kuwa bado yupo chini ya uangal­izi wa daktari Nilesh,” alisema Betty Mk­wasa.


CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic