Na George Mganga
Mwekezaji Mkuu wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji Mo, amekutana rasmi na Kocha wa Viungo wa timu hiyo, Adel Zrane kutoka Tunisia na kuweka hadharani majuku aliyompatia.
Mo ambaye alishinda tenda ya kuwekeza Simba kwa kiasi cha shilingi za kitanzania, bilioni 20, amekutana na Zrane kisha kuzungumza naye masuala kadhaa ikiwemo majukumu ambayo anapaswa kuyafanya ndani ya mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mo ameandika kuwa amempa Zrane kazi ya kuhakikisha wachezaji wa Simba wanakuwa fiti muda wote ili kuweza kuhimili mikiki-mikiki ya Uwanjani.
Aidha, Mo amemwambia Zrane anapaswa kuwapa mazoezi wachezaji wa klabu hiyo ili waweze kuwa imara wakati wote kuondoa ule ulegelege wa kuchoka kabla ya dakika 90 kumalizika.
Wakati Mo akikutana na Kocha huyo wa viungo, kikosi cha Simba kinaondoka leo kuelekea jijini Mwanza tayari kwa kucheza na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ngao ya Hisani utakaopigwa kesho Agosti 18 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
0 COMMENTS:
Post a Comment