August 17, 2018


Uongozi wa klabu ya Mbeya City umefunguka kuhusiana kukosekana kwa mdhamini mkuu wa Ligi Kuu Bara mpaka sasa.

Kwa mujibu wa Radio One, taarifa za ndani kutoka Mbeya zimesema kitendo cha mdhamini kushindwa kupata mpaka sasa kwa namna moja ama nyingine kitakuwa kimewaathiri wao.

Klabu hiyo imesema baadhi ya mambo yatakayowapa wakati mgumu ni pamoja na gharama za safari kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine ambazo zilikuwa zikitolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom ambayo mkataba wake umeshamalizika.

Aidha, mabosi wa klabu hiyo wamesema hali ya kifedha kwao imekuwa si nzuri licha ya kuwa na wadhamini kadhaa ambao wamekuwa wakiisaidia timu yao.

Wakati Mbeya City wakilalamika juu ya kukosekana kwa wadhamini, hivi karibuni iliripotiwa wapo kwenye mchakato wa katika mfumo wa Kampuni ambao utaweza kuifanya timu iendeshwe kisasa zaidi.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic