August 29, 2018


Wachezaji, wakufunzi na wafanyakazi wengine wa Manchester United wanaamini Jose Mourinho atafutwa kazi iwapo atashindwa mechi nyingine moja. (Daily Mail)

Maafisa wakuu wa klabu hiyo hata hivyo bado wana imani kwamba Mourinho, 55, anaweza kubadilisha mambo katika klabu hiyo hata baada ya United kushindwa mechi mbili kati ya tatu za kwanza Ligi ya Premia kwa mara ya kwanza tangu 1992-93.

Real Madrid wanamtaka mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling, 23, ambapo klabu hiyo ya La Liga inatarajiwa kumfuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa England uwanjani Wembley akicheza mechi ya Ligi ya Mataifa ya Uefa mnamo 8 Septemba. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Ufaransa kutoka Arsenal Alexandre Lacazette, 27, ameanza kufikiria kuhusu mustakabali wake katika klabu hiyo ya Emirates. (le10sport)


Winga wa Liverpool Sheyi Ojo, 21, anakaribia kujiunga na klabu ya Stade de Reims ya Ufaransa kwa mkopo kwa kipindi kilichosalia msimu huu. Hii ni baada ya raia huyo wa England kueleza nia ya kutaka kuhamia ligi kuu ya Ufaransa, Ligue 1. (Mirror)

Kiungo wa kati wa zamani wa Manchester City Yaya Toure, 35, anakaribia kujiunga na klabu moja ya London. Hii ni baada ya mchezaji huyo wa zamani wa Ivory Coast kupitia vipimo vya kiafya, wakala wake amesema. (Twitter)


Real Sociedad wanataka kumchukua mshambuliaji wa Everton raia wa Uhispania Sandro Ramirez. Mchezaji huyo wa miaka 23 alihamia Goodison Park majira ya joto yaliyopita lakini akatumwa Sevilla kwa mkopo. (Marca)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic