MWANACHAMA YANGA AIBUA SUALA LA UCHAGUZI, AGUSIA NAFASI YA MWENYEKITI
Wakati kikosi cha Yanga kikianza mbio za ubingwa leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya Mtibwa Sugar, baadhi ya wanachama wa klabu hiyo wameanza kuhoji juu ya uchaguzi ambao unapasw kufanyika kujaza nafasi za waliojiuzulu.
Mwanachama mmoja anayejulikana kwa jina la Edgar Chibula, amefunguka na kuelezwa kushangazwa na mchakato wa uchaguzi huo kuwa kimya mpaka sasa wakati tayari Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeshatoa siku 75.
Kwa mujibu wa Radio One, Chibula amesema viongozi wa Yanga wamekuwa kama wamelala wakati siku zinaenda na hakuna chochote ambacho kinaendelea mpaka sasa ili kuwapata mbadala wa wale walioachia ngazi.
Ikumbukwe hivi karibuni baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji walijiuzulu pamoja na nafasi ya Katibu Mkuu huku ile ya Mwenyekiti ikiwa bado ipo mashakani kama kuna uwezekano wa Yusuf Manji kurejea baada ya kujiuzulu pia pamoja na ile ya Makamu Mwenyekiti.
"Mpaka sasa hakunachochote kinachoendelea na ukiangalia siku zinadidi kwenda, nawomba viongozi wa Yanga wajaribu kuliangalia hilo ili tuende sawa na matakwa ya katiba ya klabu" alisema.
We jamaa umetumwa kama umetumwa ushindwe
ReplyDeleteww saleh fala kabisa, ushaanza kutokwa na mavi sio
ReplyDelete