August 14, 2018


Na George Mganga

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limewatangaza marefa watakaochezesha mtangane wa mechi ya Yanga dhidi ya USM Alger.

Yanga itashuka dimbani kunako kunako Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kukipiga waarabu hao kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika mjaira ya jioni.

Marefa hao kutoka nchini Namibia ni Jackson Pavaza ambaye atashika filimbi huku akisaidiwa na Matheus Kanyanga pamoja na Tauhulupo Shaanika.

Yanga itakuwa inaingia Uwanjani kucheza na USM ikiwa na kumbukumbu za kupoteza mechi ya awali kwa mabao 4-0 huku ikiwa ina alama moja pekee kundi D.

Katika kundi hilo Yanga imeambulia alama moja pekee baada ya kutoka suluhu tasa ya 0-0 na Rayon Sports ya Rwanda nchini huku ikifungwa mechi mbili mfululizo na Gor Mahia FC ya Kenya na ikipoteza mechi ya kwanza dhidi ya USM Alger.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic