ATLETICO YAIPA KIPIGO CHA MAANA REAL MADRID NA KUBEBA UEFA SUPER CUP
Real Madrid imekubali kichapo cha mabao 4-2 dhidi ya Atletico de Madrid katika mchezo wa UEFA Super CUP.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa A. Le Coq Arena, Real Madrid walifanikiwa kupata mabao yao yakifungwa na Sergio Ramos kwa njia ya penati na Karim Benzema.
Atletico de Madrid wao wamepata mabao yao kupitia kwa Diego Costa aliyetupia mbili kambani, Saul Niguez na Koke aliyefunga katika dakika ya 104.
Picha zaidi zipo hapa Uefa Super CUP
0 COMMENTS:
Post a Comment