August 16, 2018


Baada ya kumaliza kambi ya wiki mbili Kampala, Uganda, kikosi cha Azam kinarejea leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa ligi.

Azam walikuwa ya Uganda kwa maandalizi maalum ya Ligi Kuu Bara msimu ujao ambao pazia lake linafunguliwa Agosti 22 2018.

Wakati kikosi kikiwa Uganda, Azam walifanikiwa kucheza mechi za kirafiki tatu ambapo waliweza kwenda sare ya 1-1 na Express, 0-0 na URA huku wakipoteza kwa mabao 4-2 dhidi ya KCCA.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa timu hiyo Jaffer Idd Maganga, amesema kambi ya Uganda imekuwa ya mafanikio huku akiahidi kuwa wataonesha upinzani wa kutosha pale ligi itakapoanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic