August 4, 2018


Kiungo nyota wa zamani wa Uholanzi, Clarence Seedorf ameteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Cameroon.

Baada ya kuteuliwa, haraka Seedorf amemteua Patrick Kluivert waliyecheza naye Ajax na baadaye timu ya taifa kuwa kocha msaidizi.

Waziri wa michezo wa Cameroon, Pierre Ismael Bidoung Mkpatt, ndiye aliyemtangaza Mholanzi huyo aliyewahi kung’ara na AC Milan ya Italia kuwa kocha mkuu.
Taarifa za mwanzo zilieleza Cameroon walikaribia kuingia mkataba na Kocha wa zamani wa England, Sven-Goran Eriksson, raia wa Sweden amabye walishindwana mwishoni.


Baada ya hapo, wakaamua rasmi kumtangaza Seedorf kocha wa Cameroon ambayo ilibeba ubingwa wa Afrika mwaka jana, lakini ikashindwa kufuzu kucheza Kombe la Dunia nchini Urusi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic