Valencia ya Hispania imeitwanga Everton kwa mabao 3-2 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa Goodson Park jijini Liverpool.
Mechi hiyo ilikuwa ni kujiweka vizuri na msimu mpya wa 2018/19 na wenyeji Everton walionyesha matumaini mapema lakini mwisho wakashindwa kuthibiti mikiki ya wageni wao kutoka Hispania.
0 COMMENTS:
Post a Comment