Kikosi cha Simba kimeibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa huko Uturuki dhidi ya F.C.E Ksaifa.
Mabao ya Simba yamewekwa kimiani na wachezaji Emmanuel Okwi aliyefunga mabao mawili pamoja na Meddie Kagere aliyingia kambani mara moja.
Bao pekee la Ksaifa ambayo nayo ipo Uturuki kwa kambi maalum ya kujiandaa na msimu mpya, limewekwa kambani na Nader Alkrinaui.
Simba wanatarajia kuanza safari ya kurejea Tanzania kuanzia kesho kwa ajili ya tamasha la Simba Day litakalofanyika Agosti 8 2018.
Mnyama anaanza kazi huyo. Nani wa kumzuwia. Ukimuona mwenzio ananyolewa nawe haraka tia kichwa chako sabununi usiuone uchungu wa uwembe
ReplyDeleteSIMBA wale mwaka huu yetu macho ila si wa mchezo mchezo.
ReplyDeleteDah safari hii watapata tabu sana
ReplyDeleteHiyo timu ya vijana wa Kipalestina jamani sio kipimo halisi
ReplyDeleteNimeangalia mechi ya Asante Kotoko na Hearts of Oark. Timu zote ni nzuri niwaombe Simba wasifanye masihala wacheze kweli mpira ndipo ushindi upatikane.
ReplyDeleteNi vyema tukajiuliza hawa ni waarabu kutoka wapi? F.C.E Ksaifa ni timu kutoka Palestina. Tafuta kiwango cha Palestina katika hii dunia kwenye kandanda.
ReplyDelete