SIMBA WAWASILI MWANZA TAYARI KUKIPIGA NA MTIBWA, BOCCO AREJEA
Kikosi cha Simba kimeondoka jijini Arusha asubuhi ya leo kuelekea Mwanza tayari kwa mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Mtibwa Sugar.
Simba watacheza na mabingwa hao wa Kombe la Shirikisho Tanzania kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kesho majira ya saa 10 kamili jioni.
Wakati Simba wakikwea pipa na sasa wakiwa tayari wameshawasili Mwanza, taarifa zinaeleza kuna uwezekano mkubwa wa Nahodha wake, John Bocco kucheza mchezo huo.
Bocco hajacheza mechi yoyote tangu kumalizika kwa ligi msimu wa 2018/19 kutokana na kupatwa na majeraha lakini kuna uwezekano akacheza dhidi ya Mtibwa hiyo kesho.








Hii picha inavuyia zaidi kuitizama na kinachopendezesha machoni zaidi kunako hii picha ni "the wings of Kilimanjaro " .Mungu ampe maisha marefu alieamua kulifufua shirika letu la Ndege Amin.
ReplyDeleteTFF NAWAOMBA ANGALIENI NGAO HIYO. KUNA MAKOSA KATIKA MAANDISHI. IMEANDIKWA - COMMUNITY SHEILD 2017-2018. NENO SAHIHI NI SHIELD NA SIO SHEILD. FANYENI MASAHIHISHO.
ReplyDelete