TAMBWE: MAKAMBO NI ZAIDI YA NGOMA
Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe amewataka wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kutokuwa na wasiwasi na uwezo wa mshambuliaji wao mpya raia wa DR Congo, Heritier Makambo na amewahakikishia kuwa yupo vizuri zaidi ya alivyokokuwa Mzimbabwe, Donald Ngoma ambaye sasa yupo na kikosi cha Azam FC.
Tambwe ambaye ana rekodi nzuri ya kuzifumania nyavu klabuni hapo tangu alipojiunga timu hiyo msimu wa 2014/15 akitokea Simba, amefikia hatua hiyo baada ya baadhi ya mashabiki wa timu hiyo kuufananisha uwezo wa Makambo na ule aliokuwa nao Ngoma wakati akiitumikia timu hiyo.
“Mwili wake (Makambo) umeonekana ‘kunoki’ kutokana na mazoezi magumu ambayo alikuwa akifanya tulipokuwa Morogoro. Anahitaji mechi nyingine mbili za ushindani ili aweze kuwa sawa, kwa jinsi ninavyomuona atafanya mambo makubwa zaidi ya alivyokuwa Ngoma.
“Anajua kupiga mashuti, anajua kufunga kwa kichwa na miguu, ana uwezo wa kukaa na mpira, anajua kutengeneza nafasi za kufunga lakini pia siyo mchoyo na kutoa pasi za kufunga kwa wenzake, lakini pia ana kasi kubwa na nguvu za kupambana na mabeki, kwa hiyo mashabiki wampatie muda tu, naamini wote tutafurahia kutokana na uwezo wake,” alisema Tambwe.
WEWE LINI UTARUDI UWANJANI TUMEKUMISS
ReplyDeleteMakambo zaliboro..
ReplyDeleteAmisi amekwisha na aaliyombakilia nayo kuisifu yanga na wachezaji wake ili aonekane ana mahaba na timu yake ili wambakize apewe fupa kama alivo Canavaro, lakini amekwisha na ingekuwa bado anajiweza kwanini asiitwe kuichezea timu yao ya taifa kama ilivo kwa Haruna na Kagere?
ReplyDelete:d :d Shabiki wa kitanzania halisi. Kujisahaulisha ni jadi yetu. Tumeshasahau kuwa Tambwe alikuwa majeruhi na tumesahau akipotemwa simba alikuwa kaisha watu wakavunja viti1!! Kama inavyosemwa Kagere mzee tusubiri muda
DeleteNa kila muda ukipaa na Kagere anapaa nao kwa ubora wake. Si mlimtaka pamoja na Salamba na Wawa lakini wote pamoja wkachaguwa kwa Moo wa Simba kwenye kila ya uhakika?
ReplyDelete