Beki Mcolombia, Yerry Mina atalazimika kusubiri mwezi mzima ili kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha Everton.
Hii inatokana na yeye kuwa majaeruhi tokea amejiunga na Everton akitokea FC Barcelona ya Hispania.
Mina aliumia wakati wa michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika nchini Urusi akiwa anaitumikia Colombia.
Everton walimwaga pauni milioni 28.5 kupata saini yake lakini ameendelea kukaa nje wakati EPL ikiendelea.
Lakini Everton FC inayodhaminiwa na SportPesa ndiyo imetoa ufafanuzi kuhusiana na beki wake huyo mpya.
0 COMMENTS:
Post a Comment