UONGOZI YANGA WATOA TAMKO LINGINE KUHUSIANA NA KIBALI CHA KOCHA ZAHERA
Na George Mganga
Uongozi wa Yanga umesema kuwa suala la kibali cha Kocha wao Mkuu, Mwinyi Zahera bado lipo kwenye utawala likifanyiwa kazi.
Zahera tangu awasili nchini mpaka sasa hajapatiwa kibali cha kazi na mabosi wa klabu hiyo na ikiletea sintofahamu kutokana na kuendelea kukaa jukwaani wakati timu ikiwa inacheza.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mashindano, Hussein Nyika kupitia Radio EFM, amesema mchakato wa kupata kibali hicho si wa kukurupukia, bali unaendelea kwa kufuata taratibu.
Nyika amesema bado wao kama uongozi wanaendelea kufuatilia kibali hicho ambacho kinaonekana kuleta shida maana ni miezi kadhaa tayari imeshapita na hakijapatikana.
Kutokana na mchakato wa kusaka kibali chake ukiendelea, kuna uwezekano mkubwa pia leo Zahera anaweza akakosekana kwenye benchi la ufundi wakati Yanga ikishuka majira ya saa 12 za jioni kukipiga dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ikumbukwe Zahera aliwasili nchini kuchukua mikoba ya aliyekuwa Kocha wa Yanga, Mzambia George Lwandamina, ambaye aliondoka kurejea katika timu yake ya zamani, Zesco United.
Mnashindwa nini kupata kibali miezi sasa, wenzenu mbona wanaweza?
ReplyDelete