WEMA: MAJUTO AMEONDOKA NA NDOTO YANGU
Muigizaji wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu amefunguka kuwa nguli wa filamu za vichekesho marehemu Amri Athuman ‘King Majuto’ amefariki wakati akiwa hajatimiza ndoto naye aliyokuwa nayo.
Wema alisema, alipanga mwaka mmoja uliopita ilikuwa afanye kazi na mzee huyo lakini ilishindikana kutokana na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua hivyo ikabidi avute subira lakini bahati mbaya Mungu alimchukua kabla hawajafanya kazi pamoja.
“Nilipopata taarifa tu ya msiba niliumia sana, nilijua wazi kabisa ndoto yangu imezimika na kile nilichokitarajia hakikuweza kufanikiwa kabisa nilitamani kujipima nione nikicheza filamu ya vichekesho na yeye ingekuwaje lakini ndiyo hivyo tena imeshindikana,” alisema Wema.
0 COMMENTS:
Post a Comment