YANGA KUKIPIGA NA TIMU DARAJA LA PILI KILOMBERO LEO KUPATA KIPIMO CHA KUWAMALIZA WAARABU
Kuelekea mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger Agosti 19 kwenye Uwanja wa Taifa, Yanga inashuka dimbani kukipiga na Mkamba Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la Pili.
Yanga watashuka na dimbani majira ya saa 10 kucheza na Rangers katika Uwanja CCM Mkamba uliopo mjini Kilombero ili kukikipa kikosi kuelekea mechi dhidi ya waarabu.
Uongozi wa Yanga umeamua kukipelekea kikosi Morogoro kwa ajili ya kuongeza zaidi idadi ya wafuasi wake kutokana na kuwa na mashabiki wengi ambao wanaipenda klabu Yanga.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema lengo kubwa la kucheza na timu hiyo ya Daraja la Pili ni maandalizi kuelekea mechi na USM Alger ambayo itafanyikia Dar es Salaam.
si ajabu...timu zote imekuwa ikijipima nazo sijui ni za daraja la ngapi. wanashinda 1-0, .halafu tunasikia wako kamili.
ReplyDeleteKwani Dotto nao si kama hao ila kwao ni kabati tu
DeleteKitaalam ili kukipa kikosi chako uimara na kujiamini katika mifumo mbalimbali ni lazima uanze na timu za chini wakati unapanda kidogokidogo. Yanga SC haipo tena katika mazwazo ya kimataifa ila inawaza ligi na maandalizi yake mengi yapo kwenye ligi. Wachezaji wengi wapo kwa maandalizi ya ligi kwa kuwa wengi wanaoanza hasa kipande cha mbele ni wageni. Ndio maana hata wenzetu huko Ulaya utaona wanacheza na timu za Philipino, Indonesia na Asia. Kikubwa ni kuangalia mfumo kama unaweza kufanya kazi na si mmefunga magoli mangapi. Timu nyingi ukiangalia katika majaribio zimefungwa sana...FC Barcelona imefungwa sana tu...tatizo si ubovu wa timu...ila ni kitu gani mwalimu anaangalia katika timu
ReplyDelete