August 4, 2018


Na George Mganga

Klabu ya Yanga imevunja rasmi mkataba na kipa wake Mcameroon, Youthe Rostand baada ya kufikia maelewano baina yake na uongozi wa timu hiyo.

Yanga wameamua kumalizana kwa staili hiyo na Rostand ambaye amekuwa akitupiwa lawama na asilimia kubwa ya mashabiki wa Yanga juu ya kiwango chake akiwa langoni.

Kutokana na kiwango chake kushuka tofauti na wakati akisajiliwa kutoka African Lyon ya jijini Dar es Salaam, Rostand alionekana kuwa na umahiri mkubwa wa kucheza mipira ya ya mwisho kutoka kwa washambuliaji wa timu pinzani.

Hatua ya kuvunja mkataba na Rostand imekuja mara baada ya kipa huyo kukataa kupelekwa kwa mkopo katika klabu yake zamani (African Lyon) kabla hajatua Yanga na badala yake alitaka vema mabosi wake wakimlipa fedha zake ili avunje mkataba.

Baada ya kuachana na kipa huyo, Yanga sasa inasalia na makipa watatu ambao ni Beno Kakolanya, Klaus Kindoki na Ramadhani Kabwili.

Wakati Rostand akimalizana na Yanga, kikosi cha timu hiyo hivi sasa kipo mjini Morogoro ambapo kinajiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger ya Algeri autakaopigwa Agosti 19 2018 jijini Dar es Salaam.

1 COMMENTS:

  1. Kutokulipwa mishahara ni sababu kuu ya kuathiri kiwango chake na pindi angekubali kurejea timu yake ya mwanzo kiwango chake kingerejea. Unaona katika yimu hata wale walookuwa na viwango vya juu, bila ya kutaja majina sasa vimepotea nao hubadilishwa baada ya dakika chache za mchezo kwakuwa hawakuyapata waliyotegemea

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic