SIMBA KUONGEZA WENGINE SITA WAPYA
Wakati Simba ikiboreshwa zaidi kwa kikosi cha wanaume, uongozi wa klabu hiyo umesema sasa utaanza kukiimarisha timu ya Simba Queens ili kuleta ushindani zaidi.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara, amesema mipango iliyopo hivi sasa ni kuhakikisha wanasajili wachezaji wenye uzoefu.
Manara ameeleza kuwa uongozi kwa sasa upo kwenye mipango ya kuongeza wachezaji 6 ambao watakuwa msaada mzuri ndani ya Simba Queens ili kiweze kuendana na hadhi ya timu hiyo.
Kiongozi huyo amesema mchakato uliopo hivi sasa ni kusajili wachezaji hao sita kutoka kikosi cha timu ya taifa ya wanawake ambao klabu inaamini ndiyo watakuwa chachu ya mafanikio kwa klabu hiyo.
Mbali na usajili wa wachezaji hao, kwa upande mwingine Manara amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi Agosti 8 katika Uwanja wa Taifa kwa ajili ya tamasha la Simba Day ambapo Simba SC itacheza dhidi ya Asante Kotoko kutoka Ghana.
0 COMMENTS:
Post a Comment