September 24, 2018


Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi, Nape Moses Nnauye amenusurika kifo baada ya gari aina ya Land cruiser VX lenye namba 349 DEL alilokuwa amepanda kupinduka majira ya saa 1:00 asubuhi  ya leo, Jumatatu Septemba 24, 2018 katika Kijiji cha Kibutuka, wilaya Liwale, mkoani wakati akielekea Liwale kwenye ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dk.Bashiru Ali.

Imeelezwa kwamba, pamoja na Ziara ya Dkt. Bashiru, pia Nape alikuwa akienda Liwale kwa ajiri kushiriki Kikao cha Halmashauri Kuu CCCM Mkoa wa Lindi.

Nape alikuwa ameambatana na watu wengine wanne ambao wote ni wazima na hakuna mtu aliyedhurika lakini gari ndilo limeharibika kwa mbele.  Mbunge Nachingwea, Masala amethibitisha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic