September 24, 2018


Baada ya kufanikiwa kuingia mara mbili kambani jana dhidi ya Singida United, Mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Mrundi Amis Tambwe amesema hana hofu na Simba.

Tambwe ambaye aliwahi kuichezea timu hiyo miaka kadhaa iliyopita amesema hana hofu nao na kuuchukulia mchezo huo kuwa mwepesi zaidi kwake.

Mshambuliaji huyo ambaye alishawahi kuwa mfungaji bora misimu kadhaa iliyopita akiwa Simba, amesema watani zao ni wepesi na akitamba kuwa hakuna mechi nyepesi kama wanapokutana na Simba kwenye ligi.

Aidha, Tambwe amesema imekuwa ni kawaida kwa timu nyingi kuikamia Yanga inapocheza lakini anaamini kuelekea Septemba 30 lazima wapate alama tatu dhidi ya Simba.

Simba na Yanga zitakutana kwenye mchezo huo kuendeleza safari ya kuwania alama tatu Septemba 30 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic