DJUMA ABAKI SIMBA KWA MASHARTI MAGUMU
Wakati sakata la Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma kutaka kufukuzwa ndani ya kikosi cha timu hiyo likiwa bado halijapoa sana, taarifa mpya ni kwamba kocha huyo amepewa masharti magumu ambayo anatakiwa kuyafuata ili kulinda kibarua chake hicho.
Masharti ambayo Djuma raia wa Burundi amepewa ni ya kuhakikisha anafuata utaratibu wa klabu hiyo pamoja na kushirikiana vema na makocha wenzake na kusahau tofauti zao zilizopo.
Chanzo kutoka ndani ya Simba, kimeliambia Championi Jumamosi kuwa, mwekezaji na mwanachama wa klabu hiyo, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’, ndiye amezuia zoezi hilo la kutimuliwa kwa Djuma huku akitoa masharti hayo.
Chanzo hicho kilienda mbali zaidi na kueleza kuwa, awali Mo Dewji pamoja na viongozi wa juu wa Simba ndio waliokuwa kwenye mpango wa kumtimua kocha huyo, lakini baada ya taarifa hizo kuvuja, wakabadili mawazo.
“Mo ameamua kumuacha Djuma aendelee na badala yake amepewa masharti magumu ya namna ya kuishi karibu na makocha wenzake na lile suala la sare za timu ametakiwa kuhakikisha anazivaa muda wote hadi mkataba wake utakapoisha.
“Mo ameona asimtimue kwa sasa baada ya siri hiyo kuvuja kwani walitaka wafanye kimyakimya, lakini kutokana na siri kuvuja huku pia akimkosa mtu aliyetoa siri hizo, wameamua kubadili mawazo,” kilisema chanzo chetu.








Huna jipya uswahili tu. Unawenza mtimua mtu kwa siri?angalia post zako maana tunachoka nahabari zisizo na mashiko
ReplyDeleteKenge huna jpyaa....story za kutungaa ili upate rzik...daaa waandishii wa bongoo
ReplyDeleteNi rahisi sana kujiita/kuwa mwanahabari,ila ni jambo gumu sana kuwa mwanahabari mahiri,hii blog ina habari za kipumbavu zaidi ya upumbavu wenyewe!Haiangalii habari zenye maslahi kwa mustakabari wa Mpira wetu,imekuwa ikiungaunga taarifa nyingi ili ku-create negativities katika mpira wetu.
ReplyDeleteKwenye siasa hawaangalii ukweli,wanaangalia athari za habari yenyewe kwa umma,tuna mfano wa Gazeti lililowahi kuripoti kwa ushahidi kabisa,likiorodhesha hadi namba za simu na kuchapisha hadi muda wa mawasiliano na mtiririko wake,likitoa hadi miamala ya kifedha juu ya uhalifu uliofanywa na wapambe wa dola,lakini vyombo hivyo vilifungiwa.
Si kila habari ni habari,ndiyo maana kuna meza za uhariri ktk kila nyumba ya habari,pamoja na mambo mengine,meza hizo hutathmini athari za habari kabla ya kuzitoa kwa umma.
Matatizo na misuguano ya kiutendaji ni jambo la kawaida katika taasisi yoyote ile,hata huko global ulipo kuna changamoto zake,mbona hujawahi kutoa gazetini misuguano ya kiutawala ya ofisini kwenu?
Ya utawala waachieni simba,sisi tuishie tu kusapoti Yale yenye muelekeo wa kukuza soka letu,uandishi mamluki unaotumika kuchochea migogoro ya vilabu hauwezi kuwa mualobaini wa soka letu,badilikeni.
Champions wanaandika habari za upuuzi hususan zinapokuwa zinawahusu Simba.Champions ni wapuuzi
ReplyDeleteKuwasusa hawa makanjanja ndio dawa. Eti habari zimevuja. Zimevuja my foot.Championi wakiongozwa na huyo mbabaishaji wao Saleh Ally walituaminisha kwamba habari hizo ni kweli wakisema wana secret sources ambazo hawawezi kuzifichua. Imebainika kwamba ni uzushi wanakuja na face lifting ya hadhi ya gazeti lao kwa kuzua
ReplyDeleteuongo mwingine. Mimi nimeamua kuacha kusoma glo blogu na pia gazeti lao kuanzia leo na nawaomba wanasimba wenzangu tuwasusie.
Mmmh jamani hizi habar zingine mbona mnatuchanganya mara hakuna lolote mara masharti ndyo nini sasa
ReplyDeleteMnajikosha tu baada ya kuabika pumbav zenu, igine mfano wa bin zubeiry achen porojo na kijarida chenu cha champion, naona sa hv mnaandika hadi habar zisizo husiana na michezo manake mshakosa mvuto wa kimichezo..!
ReplyDeleteNi masaa tano tangu Simba iwafunge AFC Leopards.hamjaandika chochore.Ingekuwa ni habari za upuuzi au Yanga wameshinda Leo mngekuwa mmeishaandika hapa. Leo mmeandika kikosi cha Simba dhidi ya AFC Leopard.Nina hakika kesho mtaandika kwa maneno hata: KIKOSI CHA MAANGAMINZI AU CHA MAUAJI cha YANGA dhidi ya African Lyon.Acheni zenu.wapuuzi nyie.FAKE NEWS!
ReplyDeleteNaunga mkono kuwasusia .Hawana maana.Na mimi naanza kesho. Nasoma Bin Zuberi tu kuanzia kesho.
ReplyDeleteWapuuzi tena sana..walijua Simba itacheza na AFC na wakaandika majina ya Kikosi cha Simba.Wameamua kupotezea matokeo ya Mechi hiyo..itakuwa yamewaumiza saana.Ama kweli Saleh ni blog ya uzushi na udaku!Hawafai
ReplyDeleteAIBU TUPU UONGO UONGO UTADHANI NI SIFA
ReplyDelete